Banda bora la kulelea vifaranga vya kuku

Banda bora la kulelea vifaranga vya kuku смотреть последние обновления за сегодня на .

Banda Bora la Kulelea Vifaranga vya Kuku

54264
401
55
00:06:00
14.08.2019

Ili kupunguza changamoto za vifo kwa vifaranga vya kuku ni muhimu kuandaa banda bora la kulelea vifaranga vya kuku. Kutokana na changamoto hizo Shas kuku farm imebuni bruda maalum kwa ajili ya kulea vifaranga vya kuku ambalo litazuia mpaka mbu kuingia bandani ili kupunguza maambukizi ya virusi vya ndui. Tazama video hii mpaka mwisho ili uweze kujifunza kitu kwa ajili ya vifaranga vya kuku wako. Usisahau ku-subscribe kwenye channel hii #ufugajiwakuku #changamkiafursatv

Njia Rahisi Ya Kutengeneza Bluda Bora La kulelea Vifaranga Linaloepusha Magonjwa.

601
6
4
00:06:00
20.08.2022

Katika Video Hii tumekuonesha vifaa Vinavyohitajika na Chanzo Cha Joto. Karibu

UJENZI WA BANDA: La kulelea Vifaranga vya kuku aina zote "Bora na Nafuu Sana"

2276
1
00:14:47
11.01.2022

Video hii imeeelezea na kuonesha kwa kina ujenzi wa banda bora kwaajili ya kukuzia vifaranga wa kuku. Banda hili halija gharami kiasi chochote kwa sababu malighafi zilizotumika ni mkusanyiko wa masalia ya mbao na mabati ambayo yalikua hayatumiki tena. Kama unapenda kutengenezewa banda la dizaini hii, wasiliana nasi kupitia mawasilino hapo chini. #UjenziWaBanda #Kuku CONTACT US EMAIL: RUBABAIMANI🤍GMAIL.COM PHONE: +255(0) 764148221 SUBSCRIBE KUJIFUNZA MENGI ZAIDI

MAMBO 5 MUHIMU KATIKA UJENGAJI WA MABANDA YA KULELEA VIFARANGA

2074
42
8
00:04:53
07.06.2020

#kukuchapchap #KUROILERS #Banda #Vifaranga Banda bora ndilo msingi na ndio chanzo kizuri cha ukuaji wa VIFARANGA/KUKU wako vizuri, Hivyo basi kama hutozingatia ujengaji bora wa banda na kuhakikisha unafuata kanuni bora na nzuri katika utengezaji bora wa mabanda utakua unakosea na kujisababishia hasara nzuri tu katika mradi wako wa kuku. 🤍am/kuku_chapchap 🤍ok/kuku_chapchap

Banda bora la Vifaranga 1200 - 1500 wa Kienyeji, Chotara, lenye kupunguza gharama za kulea hadi 5%

36223
295
129
00:11:31
17.10.2019

#Banda bora la #Vifaranga 1200 - 1500 wa #Kienyeji, #Chotara, na #layers lenye kupunguza gharama za kulea hadi 5%

SIFA ZA BANDA BORA LA VIFARANGA VYA KUKU WA KIENYEJI

7108
75
7
00:09:35
28.01.2020

#banda #vifaranga #kienyeji

Ujenzi wa Banda la Vifaranga wa Kuku wa Kienyeji

82054
471
71
00:09:52
07.09.2021

Ujenzi wa banda la kutunzia Vifaranga wa Kuku wa kienyeji. Ili vifaranga wa kienyeji wakue bila changamoto za vifo kama mfugaji wa kuku haupaswi kusahau ujenzi wa banda la kulelea vifaranga. Banda la vifaranga ni sehemu muhimu sana katika ufugaji wa kuku wa kienyeji. Vifo vingi vinavyotokea kwenye kuku wa kienyeji ni kwa sababu ya wafugaji hawaandai banda la kulelea vifaranga hivyo wanawaacha kuku wazunguke na vifaranga wao mchana kutwa bila kufikiria hatari ya wanyama na ndege wa porini waonaowahitaji hao vifaranga kama kitoweo. Sasa kwenye makala ya leo tutajifunza Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa ujenzi wa banda la kulelea vifaranga wa kienyeji. #jinsiyakutengenezabandalavifarangawakienyeji

MABANDA YA KISASA YA KULELEA VIFARANGA

9215
42
12
00:02:10
21.05.2019

MABANDA YANYE MAZINGIRA WEZESHI NA RAHISI YENYE KUPUNGUZA CHANGAMOTO ZA MAGONJWA KWA VIFARANGA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 90 MUUNDO NA UTENGENEZAJI UMEFANYWA NA "ASK INCUBATORS TZ" WAWEZA TEMBELEA KURASA ZETU "ASK INCUBATORS TZ" -TWEETER -INSTAGRAM -FACEBOOK -NA YOUTUBE CHANEL YETU WASILIANA NASI KUPITIA +255717523626 CALL/WHATSAPP

Namna ya Kusafisha Banda la Vifaranga vya kuku

4604
28
5
00:02:07
30.03.2020

Tambua njia Nzuri ya kusafisha banda la Vifaranga vya Kuku #MzunguwaKichaga #Kuku

JIFUNZE KULEA VIFARANGA,maandalizi ya bruda,kupokea vifaranga na kulea vifaranga wa siku 1.

16136
99
25
00:06:57
07.03.2021

NJIA BORA YA KULEA VIFARANGA Ni jambo la kuzingatia kwamba vifaranga (Umri wa siku moja) wanapata joto la kutosha katika majuma matatu ya mwanzo wa maisha yao, vinginevyo watakufa. Ni lazima waangaliwe vizuri, watunzwe katika hali ya usafi na kulishwa kikamilifu ili waweze kutoa matunda mazuri hapo baadaye. KUANDAA CHUMBA AU BANDA LA KULELEA VIFARANGA Usafi ni jambo la lazima, chumba au banda ambapo vifaranga watawekwa sharti lisafi shwe kwa kusuguliwa mara mbili au tatu kwa kutumia sabuni au maji. Kabla ya vifaranga hawajawekwa ndani liwe limekauka vizuri. Vyombo vya kulishia chakula na kunyweshea maji pia vioshwe viwe safi . • Mlango wa sehemu ya kulelea vifaranga ifungwe vizuri kuzuia upepo kuingia, pawepo na vidilisha angalau viwili kwa kuingiza hewa na mwanga. • Sakafu ifunikwe vizuri kutumia majani makavu au malanda na magazeti kwa wiki ya kwanza kuzuia baridi. Kazi hii ifanywe siku moja kabla ya kuwasili vifaranga. • Vifaranga wanahitaji joto la kutosha siku za mwanzoni. • Kama kuna umeme basi vifaranga wapewe joto kutumia balbu yenye moto mkubwa (Infra-red lamp) kama hakuna umeme taa ya mafuta inaweza kutumika moja kwa kila vifaranga 100 ikitundikwa nchi 18 kutoka sakafuni kwa siku chache za mwanzoni. • Chakula na maji viwepo ikiwezekana kwa kutumia makasha yaliyosambazwa ili vifaranga waweze kula na kunywa kwa urahisi kuanzia siku ya kwanza. • Tumia vyombo vya kulishia chakula na kunyweshea maji vyenye vipimo sahihi. Kwa mfano chombo cha kulishia chenye urefu wa futi 3 kinatosha kulisha vifaranga 50 na chombo cha maji kimoja kwa vifaranga 25. MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUINGIZA VIFARANGA BANDANI Ingiza kasha lenye vifaranga ndani ya chumba au banda la kulelea, washa taa, vyombo vya kulishia vikiwa vimejazwa chakula na maji ya kunywa yapo. Sakafu itakuwa tayari imefunikwa na majani makavu au malanda ya mbao na kisha magazeti. Toa vifaranga ndani ya kasha na kuviweka karibu na mwanga wa taa, mara tu wataanza kula na kunywa maji. Kama kuna baadhi ya vifaranga wanaonekana kuwa wadhaifu ingiza midomo yao polepole kwenye maji mara mbili au tatu, nao wataanza kula na kunywa maji kama wengine. Funga mlango polepole kwani kelele zitawafadhaisha vifaranga, rudi bandani kuangalia wanavyoendelea mara kadhaa ili kuhakikisha kwamba hakuna walio dhaifu. Jaza vyombo vya chakula kila mara. Chakula kinapopungua na maji safi yawekwe kila siku kwa kumwaga yaliyopo na kuosha vizuri vyombo vya maji. Maji yanayojazwa yasiwe baridi sana. Chunga vifaranga kuona kama hawali, kunywa au kukimbiakimbia, kuna kasoro. Aidha kuna upepo na pengine hali ni ya joto mno au baridi sana. Baada ya siku chache pandisha taa juu kidogo, na endelea kufanya hivyo kwa muda wa siku chache. Baada ya wiki moja acha mlango wazi wakati wa joto lakini ziba mlango kwa waya ili kuzuia wanyama na watoto. Madirisha yafunguliwe wakati wote isipokuwa usiku na panapokuwa na baridi. Siku ya 7 vifaranga wapewe chanjo ya Newcastle (mdondo) na irudiwe kila baada ya miezi mitatu Baada ya siku 10 taa inaweza kuzimwa wakati wa mchana na kuwashwa wakati wa usiku tu. Hakikisha kuwa hakuna panya ambao licha ya kula chakula pia wanaweza kula vifaranga. Baada ya wiki 3 vifaranga wana nguvu za kutosha na hawahitaji tena joto la taa. Vifaranga sasa wanaweza kuhamishwa chumba kikubwa. Baada ya kuhamishia vifaranga katika sehemu mpya, sehemu ya kulelea isafi shwe kwa kuondoa takataka na kuzichoma moto. Pia vyombo vya chakula na maji kwa kusuuzwa kwa dawa (disinfenctant) tayari kwa matumizi ya mkupuo mwingine wa vifaranga wachanga. Sehemu (chumba) ya kulelea vifaranga inapaswa kuachwa kwa muda usiopungua wiki 3 kabla ya kupokea vifaranga wengine. Katika muda huo chumba kisafi shwe, kisuguliwe na kuwekwa dawa mara mbili au tatu. JINSI YA KUTAYARISHA SEHEMU YA KULELEA VIFARANGA WA KUKU WA KIENYEJI Vifaranga wachanga (umri wa siku moja) tofauti na wanyama wengine wafugwao hawawezi kuishi bila kuwepo uhakika wa joto la kutosha. Kuna njia nyingi za kulea vifaranga wachanga, lakini njia sahihi kwa wakulima wa vijijini pasipokuwa na umeme au mafuta ya taa ni kutumia kasha lililotengenezwa kutumia majani makavu, kama ifuatavyo: Katika banda au chumba kilichosafi shwa vizuri na sakafu kufunikwa majani makavu tengeneza duara yenye upana wa futi 3 kwa kutumia fito zenye urefu wa nchi 9 halafu zungushia wavu wa mbu na kuacha upana wa nchi 9. Ziba waya wa mbu kwa majani makavu na kuacha wazi mlango. Tengeneza paa la msonge kwa kutumia majani makavu ambalo litafunika vizuri duara lililojengwa tayari. Wakati wa mchana paa la msonge laweza kuondolewa kwenye duara ili vifaranga wapate mwanga na uhuru wa kukimbiakimbia. Wakati wa usiku paa la msonge sharti lirudishwe juu ya duara na mlango ufungwe kwa tofali au jiwe ili kuhifadhi joto kwa ajili ya vifaranga. Vifaranga wakishapata nguvu ihakikishwe kwamba vifaranga wanapata chakula na maji safi ya kutosha. #mkulimasmart #shambadarasa

UANDAAJI WA BANDA LA VIFARANGA WA KUKU WA NYAMA (BROILER),KIENYEJI,CHOTALA

11533
177
45
00:09:58
13.05.2020

Hii ni njia Bora ya UANDAAJI wa banda la vifaranga wa (broiler) vifaranga wa kienyeji,vifaranga wa chotara na vifaranga wa mayai.

Banda Bora la Kuku Hupunguza Changamoto

46385
250
54
00:04:41
07.11.2020

Ujenzi wa banda bora la kuku wa Kienyeji, chotara, kuku wa nyama na kuku wa mayai linavyoweza kupunguza changamoto mbalimbali za magonjwa ya kuku Banda bora ni banda ambalo linakidhi mahitaji ya kuku wako na liendane na idadi ya kuku unaofuga. Umuhimu wa banda bora; Banda bora linasaidia kupunguza changamoto za magonjwa USIBONYEZE: 🤍 Sifa za banda bora. I. Lijengwe sehemu isoyotuama maji II. Likinzane na uelekeo wa upepo na mvua III. Liruhusu mzunguko wa hewa IV. Liwakinge kuku wako dhidi ya baridi V. Liwe na vichja kwaajili ya kupumzika, kufanya mazoezi na kulala, pia Liwe na viota vya kutagia ambavyo huwekwa kuku wakifikisha miezi 3 VI. Liwe rahisi kusafishika VII. Liendane na idadi ya kuku bandani Hapa sasa watu wengi hua wanafeli na kujisababishia changamoto za magonjwa, kudonoana na kula mayai. Kuku anahitaji sehemu ya kutosha ili aweze kuwa huru na kufanya mazoezi ndio maana wanaofuga huria au nusu ndani nusu nje wanapata matokeo mazuri. Kila aina ya kuku anahitaji nafasi yake. 1m square inahitaji kuku chotara 4/5 1m square inahitaji kuku wa mayai 6/8 1m square inahitaji kuku wa kienyeji/nyama 8. Mfano unataka kujenga banda la kuku chotara 100, unachukua 100÷4=25m square au 100÷5=20m square, sasa hii 25/20m square ndio ukubwa wa banda. 25=6.25x4 na 20=5x4. Ukizingatia vipimo utapunguza changamoto.

Fanya hivi kujenga Banda bora la kuku

498
10
9
00:09:07
02.10.2022

Katika video hii uyajifunza kuhusu 1.Aina za mabanda 2.Sifa za banda bora 3.Kwanini ujenge banda bora 4.Mambo ya kuzingatia unapojenga banda bora 5.Vipimo vya banda bora Mambo muhimu mengine ya kujifunza Kwa kawaida ufugaji wa kuku unaanza kwa Kufikiria kuhusu Soko, aina ya kuku unaotaka kufuga, Banda, etc 1.Jifunze kuhusu Utafiti wa Soko👇🏽 🤍 2.Je ufuge kuku aina gani?👇🏽 🤍 3.Jifunze namna ya kujenga Banda Bora katika video hii👇🏽 🤍 4.Je mfumo gani unalipa zaidi ?👇🏽 🤍

TAMBUA NJIA BORA YA KUTUNZA VIFARANGA VYA KUKU WA KIENYEJI KWA URAISI

14145
53
1
00:03:13
01.08.2019

SUBSCRIBE Kwa maoni na ushauri tupigie kwa namba 0713442644.

BANDA BORA ENEO DOGO#Kuku Uchumi

17956
121
30
00:11:46
30.12.2021

Unaweza Kuwa na eneo dogo bado ukaweza Kufuga Kuku wengi, je inawezekanaje? Jifunze kupitia video hii.

MAMBO 9 YA KUZINGATIA KATIKA ULEAJI WA VIFARANGA KUANIZA SIKU YA KWANZA.

15207
200
22
00:06:15
10.01.2021

#Vifaranga #Vifarangavya kuku #Uleajiwavifaranga Kuku aliyetotoa vifaranga anaweza kuachiwa avilee mwenyewe, lakini ili kuweza kupata matokeo mazuri na ili vifaranga vyako vikue vizuri ni lazima utumie brooding system kuepuka majanga kama vile magonjwa, vicheche na mwewe. Facebook - 🤍 Instagram - 🤍 YouTube - 🤍 WhatsApp - +255 (0) 719 882 004 / +255 (0) 628 670 230 🤍

BANDA BORA LA KUKU CHOTARA | KIENYEJI, TENGENEZA HIVI UNUFAIKE ZAIDI FUGA KUKU WENGI.

435
1
00:01:18
10.02.2022

#bandabora #bandalakisasa #ufugajiwakuku hili ni banda la kisasa banda bora la kisasa ufugaji wa kuku tengeneza hivi unufaike zaidi asante kwa kutazama

ULEAJI WA VIFARANGA VYA KUKU CHOTARA |VIFARANGA VYA SASSO|

1323
12
13
00:06:03
10.07.2022

Vifaranga Bora Vya Kuku aina ya Sasso SASSO TANZANIA 🐣Vifaranga bora vya Kuku aina ya Sasso 🐥Vifaranga vya Siku 28,Wakiwa na chanjo zote 🐔Sasso chicken ULEAJI WA VIFARANGA. Ni kitendo cha kutengeneza mazingira ya kukuza vifaranga kwa kuwapa chakula bora na joto kwa vifaranga kuanzia wakiwa na umri wa wiki 0 hadi 6, ili ajimudu kuishi kwa joto linalohitajika, joto linaweza kupatikana kwa kutumia gesi, umeme au mkaa, eneo la bruda linatakiwa kuwa tayari masaa ishirini na nne kabla ya kufika kwa vifaranga. Kuna aina kuu mbili za uleaji wa vifaranga - Njia ya kisasa. Kwa kutumia joto litokanalo na mkaa (chungu au jiko), umeme, gesi au taa ya mafuta. - Njia ya asili. Kwa kutumia kuku jike mwenyewe. Bruda za kisasa ni kama zifutazo - Kwa kutumia chungu, chungu kimoja huweza kuhudumia vifaranga 70-150. Namna ya kutumia chungu. Washa mkaa nje ya banda na kuweka kwenye chungu au unaweza weka mkaa na kuongeza kaa la moto ili ukolee. Angalia kama mkaa unatoa moshi mwingi basi uache kwa muda nje ya banda ili ukolee na kupunguza hewa ukaa Co (kaboni oksaidi) weka bandani chungu ili kuweza kusambaza joto kwa vifaranga. Chungu ni bora sana kuliko jiko kwani hutunza joto kwa muda mrefu sana na ni salama kwa vifaranga kwa vile sio rahisi mkaa kuruka na kuunguza vifaranga kwa njia yeyote. - Kwa kutumia taa maalum za umeme, Taa moja huweza kutunza vifaranga 50 – 200. - Kwa kutumia gesi, Aina hii ya bruda hutunza vifaranga 50 – 500. - Kwa kutumia nyasi kavu, Nyasi huwekwa kwenye boksi/kiota, aina hii ya bruda hutunza vifaranga hadi 50. - Kwa kutumia taa ya kawaida, Vifaranga hulelewa/kutunzwa kwa kutumia taa ya kawaida (taa ya chemli), ambayo hupendelewa na watu wengi kwa sababu ya urahisi, Hutunza vifaranga 10 – 50 kwa kutumia taa moja. Sehemu za bruda. I) Taa/chungu– hutoa joto. II) Nguzo ya pembeni (brooder guard) huzuia vifaranga kutoka kwenye chanzo cha joto. III) Matundu yaliyopo kwenye chungu . Husaidia kuruhusu moshi kupita kutoka kwenye mkaa unayowaka na kuingiza oksijeni ili kukoleza mkaa IV) Waya, Huzuia vifaranga kusogea karibu na taa kwani wanaweza kuungua. ULEAJI WA VIFARANGA WA KIENYEJI KWA NJIA YA KISASA ULEAJI WA VIFARANGA WA KUKU WA KIENYEJI ... Utunzaji wa Vifaranga vya Kuku wa Kienyeji BILA VIFO Uleaji Wa Vifaranga Siku ya 1 - 7, Hatua kwa Hatua. Hatua ... ULEAJI WA VIFARANGA. Ni kitendo cha kutengeneza ... #mkulimasmart #shambadarasa KULEA VIFARANGA ULISHAJI VIFARANGA/CHANJO/DAWA. KANUNI SAHAHI YA ULEAJI WA VIFARANGA VYA KUKU ULEAJI WA VIFARANGA VYA KUKU ULEAJI BORA WA VIFARANGA Kanuni za uleaji wa vifaranga vya kuku MBINU BORA ZA KULEA VIFARANGA VYA KUKU | Mambo Ya kuzingatia Katika utunzaji wa vifaranga uleaji wa vifaranga pdf ulishaji wa vifaranga kulea vifaranga bila umeme vifaranga vya kuku chotara vyakula vya kukuza vifaranga haraka vifaranga vya broiler bei ya vifaranga vya kuku wa nyama 2022 matumizi ya glucose kwa vifaranga

Uleaji wa Vifaranga wa Kuku wa Kienyeji Kwa Njia ya Kisasa

25283
226
67
00:13:46
07.04.2021

Uleaji wa vifaranga wa kienyeji kwa njia ya kisasa Tukuachilia mbali mbinu ya zamani ya uleaji wa vifaranga wa kuku wa kienyeji, wafugaji walikuwa wanashindwa kuendeleza mradi kwa sababu ya vifo vingi vya vifaranga. Ili kuhakikisha mradi unakuwa, mfugaji unapaswa kulea vifaranga wa kienyeji kwa njia ya kisasa. Vitu muhimu kwenye uleaji wa Vifaranga wa Kienyeji kwa Njia ya Kisasa 1. Banda la kulelea Vifaranga wa kienyeji 2. Vifaranga vya chakula na maji ndani ya banda la Vifaranga 3. Walishe Chakula cha vifaranga chenye virutubisho vyote 4. Zingatia usafi wa vyombo na banda la Vifaranga 5. Wape antibiotics na chanjo kwa wakati. Kwa muda wote huo unaweza ukatumia Neoxychick formula au otc 20 na vitamin, Amprollium. #uleajiwavifarangawakienyeji

JIKO LA KULELEA VIFARANGA:

22
0
0
00:00:29
25.09.2021

Ni muhimu kuwakinga vifaranga wa kuku dhidi ya baridi hasa katika misimu ya barid.Chungu au jiko hili huweza kulelea au kuhudumia vifaranga karibu 100

Banda bora la kuku wa kienyeji 2021

2196
24
0
00:00:15
06.09.2021

Sifa za banda bora 1.Sehemu ya kujenga banda: Chagua sehemu sahihi isiyo na vikwazo kufikiwa na huduma kama vile watoa huduma za maji, chakula, ulinzi, wanunuzi. Mambo haya na mengine yenye kufanana na hayo ni muhimu kuzingatiwa. Epuka kujenga sehemu yenye kutuama maji utasababisha mafuriko ya maji bandani, unyevu nyevu wa mara kwa mara na magonjwa yasiyoisha hasa wakati wa mvua. 2.Uelekeo wa banda: Jenga banda pande za marefu ya banda zitizame Kusini na Kaskazini ili kuepusha tabu ya mvua, upepo na jua kupiga kuku bandani. Kitaalamu dunia hujizungusha kutoka Magharibi kwenda Mashariki na pepo huvuma kinyume na uelekeo wa dunia, hiyo pepo nyingi huvuma kutoka Mashariki kuelekea Magharibi. Mvua hunyesha kwa kutegemea uelekeo wa upepo. Aidha, jua huchomoza Mashariki na kuzama Magharibi. Kama mfugaji atajenga banda lake marefu ya banda yakaelekea Mashariki na Magharibi ajue kuwa madirisha yake yataelekea Mashariki na Magharibi, hivyo mvua itanyesha bandani, upepo utavuma na kusumbua kuku. Pia, jua litapiga bandani asubuhi na wakati wa jioni. Ili kuepukana na tatizo hili, ni vema mapana ya banda yatizame Mashariki na Magharibi na pasiwe na dirisha lolote kwenye mapana yote kuepuka adha ya mvua, upepo na jua. 3.Usalama wa kuku bandani: Hakikisha banda ni imara kuepusha wizi kwa kuvunja mlango, madirisha au kubomoa ukuta. Mfugaji anaweza kutumia wavu imara kwenye madirisha, ukuta wa tofali au miti imara na kuezeka vizuri banda lisivuje wakati wa mvua. 4.Nafasi ndani ya banda: Jenga banda kulingana na wingi wa kuku watakao ingia na kuishi humo. Nafasi nzuri katika ufugaji wa kisasa ni: kuku wa mayai wanne kwa kila mita moja ya mraba. Kuku wa kisasa wanaweza kukaa watano hadi sita. 5 – 6. Kuku wakijaa, hushindwa kula vizuri, hudumaa, kumwaga maji bandani, kupata maradhi mengi, kujenga tabia ya kudonoana na kushindwa kutaga vizuri au kula mayai kwa wale kuku wa mayai. 5.Hewa na mwanga: Kuku wanahitaji hewa safi na mwanga wa kutosha ili wakue na kuzalisha vizuri.

JINSI YA KULEA VIFARANGA VYA KUKU BILA KUPATA V I F O

87825
754
83
00:10:35
04.11.2020

Jinsi ya kulea vifaranga vya kuku bila kupata vifo USIBONYEZE: 🤍

UFUGAJI WA KUKU:Mbinu za Ujenzi wa banda bora la kuku kwa gharama nafuu

2913
13
4
00:05:21
08.09.2021

JINSI YA KUJENGE BANDA LA KUKU la gharama nafuu Kabla ya jenga banda kuna mambo muhimu ambayo mfungaji unatakiwa tayari uwe umeshayaju hata kabla ya kuchukua maamuzi ya kujenga banda. aina ya kuku unaotaka kufuga mfumo wa kufugia idadi ya kuku unaotaka kufuga lengo la kufuga AINA YA KUKU UNAOTAKA KUFUGA Ninaposema aina ya kuku unaotaka kufuga na maana ujue kama unataka kufuga aina gani kuku wa nyama/ broiler kuku wa mayai/ layer kuku wa kienyeji/ local kwa sababu kila aina ya kuku inamaitaji yake mfano ukitaka kufuga layer lazima uandae na kutengeneza sehem ya kutagia BANDA BORA LA KUKU WA KIENYEJI . BANDA BORA LA KUKU WA KIENYEJI | CHOTARA JINSI YA KUJENGA BANDA BORA LA KUKU Banda la kuku 100 wa kienyeji Banda Bora la Kuku / Fuga Kuku Wengi Kwenye Eneo Dogo BANDA BORA LA KUKU Fahamu ujenzi wa banda bora la kuku bei ya banda la kuku matandazo ya banda la kuku banda la kuku la ghorofa banda la kuku kwenye eneo dogo banda la kuku in english banda bora la kuku wa kienyeji pdf vibanda vya kuku mabanda ya vifaranga vya kuku #mkulimasmart #shambadarasa

NJIA NZURI ya Kulea vifaranga:Faida za Kulea Vifaranga vya kuku Kwa Kutumia Brooder

1468
12
3
00:03:17
11.08.2021

MAANDALIZI YA NYUMBA/BANDA LA KULELEA VIFARANGA WIKI MOJA KABLA YA KULETWA VIFARANGA; 1. Nyumba ya kulelea vifaranga ni lazima ifanyiwe usafi wiki moja kabla ya kuingiza vifaranga. 2. Baada ya kupigwa deki au kufagiliwa itawekwa dawa ya kunyunyiza na bomba [sprayer] sakafuni ukutani na upande wa ndani wa paa la nyumba. Dawa hii itasaidia kuua utitiri, chawa, viroboto na vimelea vya magonjwa mbalimbali. Dawa itatumika kadri ya maelezo ya watengenezaji. 3. Baada ya kuwekwa dawa liache banda likauke kwa wiki moja kabla ya kuingiza vifaranga. 1. KUTENGENEZA KIFAA CHA KULELEA VIFARANGA (BROODER AND HOOVER; Hiki ni kifaa maalumu cha kulelea vifaranga wasiotunzwa na mama yao. Vifaa vya kutengenezea kifaa cha kulelea vifaranga o Ceiling board na au maboksi magumu o Wavu /kizuizi cha joto kali o Chanzo cha joto [jiko la mkaana mkaa, balbu –infra-red bulb] o Takataka za mbao /mabaki ya mpunga o Magazeti, / boksi laini o Mfuniko [hoover]. Kutengeneza Brooder/Bruda ya kutunza Vifaranga Faida za Kulea Vifaranga vya kuku Kwa Kutumia Brooder *Bruda la kulelea vifaranga.* Kinga... Kulea Vifaranga vya Kuku kwa Kutumia Brooder Umuhimu Wa Bruda Kwa Vifaranga - FUGA KIBIASHARA ULEAJI WA VIFARANGA. Ni... - Vifaranga wa kienyeji Moshi ... MBINU BORA ZA KULEA VIFARANGA VYA KUKU | KILIMO ... KULEA ... - FUGA KUKU KWA NJIA YA KISASA na Majumbeni Jiko Maalum La Kutunzia Vifaranga KULEA VIFARANGA ULISHAJI VIFARANGA/CHANJO/DAWA. NJIA ZA KUTOTOLESHA VIFARANGA. Utotoleshaji wa vifaranga ... Kujua Ufugaji bora wa kuku Mfugaji anaweza kulea vifaranga wengi kwa kutumia bruda uleaji wa vifaranga pdf vifaranga kusinzia kupokea vifaranga baridi kwa vifaranga vifaranga wa mwezi mmoja joto kwa vifaranga dawa za asili za vifaranga ufungaji wa vifaranga #mkulimasmart #shambadarasa

JINSI YA KULEA VIFARANGA VYA KUKU BILA KUPATA HASARA YA VIFO

1092
11
2
00:04:42
05.10.2021

#KPTL TANZANIA#🤍

Malezi ya vifaranga wa kuku wa nyama broilers;Zingatia mambo 5 KUlea vifaranga wa broilers

976
7
2
00:03:14
06.09.2021

UFUGAJI WA KUKU BORA WA NYAMA (BROILER) HATUA KWA HATUA: kufugia ni kama inavyoonyesha hapa. 👉Mazingira yanayolizunguka banda la kuku na vyombo vyote vilivyotumiwa kwa batch iliyopita yapaswa kusafishwa vyema kwa maji safi na dawa ili kuua vimelea ambavyo vinaweza sababisha magonjwa. 👉Hakikisha sehemu ya kulelea vifaranga (brooding area) inawekewa chanzo cha joto saa moja kabla ya vifaranga kuingia ndani ya eneo la kulelea vifaranga. 👉Kwa matokeo chanya na yenye faida vifaranga wafikishe kwenye banda haraka iwezekanavyo na kama inawezekana wapewe glucose na baada ya hapo chakula. 👉Kamwe usisafirishe vifaranga kwa kutumia buti la gari mara nyingi vifaranga husafirishwa wakiwa wamewekwa kwenye kiti cha gari ambapo watapata hewa ya kutosha na kuepuka msongo (stress). 👉Nafasi ya vifaranga inatakiwa kuwa vifaranga kumi kwa mita square moja (10 chicks/1m square) epuka kuwajaza kuku wengi katika eneo dogo. 🐔Mambo ya kuzingatia baada tu ya vifaranga kufika shambani mwako: 👉Mara wafikapo tu vifaranga wanatakiwa kuondolewa kwenye boksi mara moja. Unapowachelewesha ndani ya box utawafanya kuku kuwa na stress na hivyo kupelekea vifo au kuku kutokua vizuri. 👉Kwa siku saba za mwanzo wape mwanga kwa masaa 23 ili kuwawezesha vifaranga kuzoea mazingira mapya na kuwafanya wao kula chakula. 👉Wape maji na chakula baada ya vifaranga kuingia bandani na hakikisha unaongeza vitamini kwenye maji au glucose kabla ya kuwapa hao vifaranga. 👉4. Hakikisha unapanga vyema vyombo vya chalula (feeders) na vyombo vya maji (drinkers) katika mpangalio ambao utawawezesha vifaranga kula na kunywa maji bila ya kupata shida. #mkulimasmart #shambadarasa TUNAUZA VIFARANGA WA BROILER (KUKU WA NYAMA ... UFUGAJI WA KUKU BORA WA NYAMA UFUGAJI WA KUKU BORA WA NYAMA (BROILER) HATUA KWA HATUA Broiler Broiler Broiler Vifaranga vya Broiler vinapatikana Sasa Arisefarms VIFARANGA VYA BROILER VINAPATIKANA. Kuku wa Nyama - Wikipedia, kamusi elezo huru bei ya vifaranga vya kuku wa nyama 2021 bei ya vifaranga vya kuku wa nyama 2020 bei ya vifaranga vya kuku wa kienyeji bei ya vifaranga vya kuku wa mayai ufugaji kuku wa nyama broiler pdf chakula cha broiler molasses kwa kuku ufugaji wa kuku wa nyama na gharama zake

Jinsi ya Kutunza Vifaranga vya Kuku wa Kienyeji

172279
904
132
00:08:19
18.07.2021

jinsi ya kutunza vifaranga vya kuku wa kienyeji Ufagaji wa vifaranga vya kuku wa kienyeji una changomoto nyingi, wafugaji wengi wamekuwa hawajui mbinu ambazo zitawasadia kuweza kutunza vifaranga vya kuku wa kienyeji katika mbinu ambazo zitawafanya vifaranga wasife. kama nawe ni miongoni mwa wafugaji hoa, siku ya leo nitakupa mbinu bora za kutunza vifaranga vya kuku wa kienyeji.

VIPIMO SAHIHI VYA UJENGAJI BANDA KULINGANA NA AINA YA KUKU UNAYOTAKA KUFUGA.

3600
40
5
00:05:55
14.08.2021

#BANDALAKUKU #kukuchapchap #VIPIMOSAHIHIVYAUJENGAJIBANDA KULINGANANAAINAYAKUKUUNAYOTAKAKUFUGA. Banda zuri na lenye uwiano mzuri kwa kuku ni lile banda lililo kamilika kwa vipimo stahiki kutoka na aina ya kuku unaowafuga kwa muda huo. Kwa mfano, ukubwa wa banda la kuku wa mayai au kuku wa nyama 100 ni tofauti na ukubwa wa banda la kuku chotara au kuku wa kienyeji. Connect with Kuku Chap chap on Social Media: Instagram:🤍 Facebook:🤍 chapchap Twitter:🤍 TikTok:🤍 ©️2022 Kuku Chap Chap .All rights reserved +For More Information Booking Kuku Chap Chap : Contact : +255 719 882 004 email : kukuchapchap🤍gmail.com ©️2022 kuku Chap chap All rights reserved. Music in this video Learn more Youtube Channel Kuku chap chap Licensed to YouTube

UJENZI WA BANDA BORA LA KUKU KIENYEJI | CHOTARA | MAYAI | NYAMA / BROILER

232446
1671
185
00:13:00
16.11.2019

Ujenzi wa Banda Bora la Kuku | Kuku chotara | Kuku wa Kienyeji | Kuku wa Mayai | Kuku wa Nyama. Ni video inayofundisha namna ya ujenzi bora wa kuku aina zote. Kwenye video hii utajifunza 1. jinsi ya kupata ukubwa wa banda kwa aina zote za kuku 2. Malighafi za kutumia 3. Vipimo vya urefu na upana

ULEAJI WA VIFARANGA WA KIENYEJI KWA NJIA YA KISASA

235962
2791
238
00:10:27
07.03.2020

Uleaji Bora wa Vifaranga wa kienyeji Wafugaji wa kuku wa kienyeji, wengi hulifanikisha zoezi la ukusanyaji wa vifaranga wengi wa kienyeji kwa njia rahisi. Changamoto kubwa kwao ni uleaji wa bora wa vifaranga. Kwenye video hii tutajifunza Uleaji wa vifaranga wa kienyeji kwa njia ya kisasa. kwa sababu bila kuwa na elimu ya ufugaji wa kuku vifo vingi hutokea na Wafugaji hukata tamaa. Ili Kujifunza zaidi tafadhali tazama video hii 🤍

MWALIMU KUKU KATIKA ULEAJI RAHISI WA VIFARANGA

248
2
0
00:01:23
13.01.2023

BANDA LA KULELEA VIFARANGA 300 HADI 400 BEI NI 550,000/=

Jinsi ya Kutunza Vifaranga wa Kuku Chotara (Kuroiler)

21022
181
32
00:09:06
22.08.2021

Maandalizi kabla ya kupokea vifaranga na jinsi ya kutunza vifaranga wa kuku chotara (Kuroiler) Ni vema vifaranga walelewe katika chumba maalum hadi umri wa majuma manne 1. Chumba kitayarishwe siku kumi na nne kabla ya vifaranga kuwasili kama ifuatavyo: 2. Matundu yote yaliyo kwenye sakafu, dari, madirisha na ukuta yazibwe. 3. Kama chumba hicho kina sakafu ya saruji, kisafishwe kwa maji ya moto na baadaye kinyunyizie dawa kama vile Rhino au Dettol ya kuua wadudu. 4. Mazingira ya nje ya banda yawekwe katika hali ya usafi ili kuzuia wadudu waharibifu. Kusafishwe hadi kufikia upana wa mita mbili au zaidi kuzunguka banda. 5. Katika chumba watakamofikia vifaranga tengeneza sehemu maalum ya kulelea (kitalu). Sehemu hiyo maalum inatakiwa iwe na umbile la duara, itengenezwe kwa kutumia karatasi ngumu au majamvi. Mduara huhifadhi joto, huzuia upepo na huzuia vifaranga wasiende mbali na chanzo cha joto. 6. Sakafu iwekwe matandazo yaliyopigwa dawa mfano ya kuuwa wadudu kama Municipal disinfectant. 7. Matandazo yaweza kuwa pumba ya mpunga, maranda ya mbao, nyasi n.k.

Banda bora la kuku

2058
8
1
00:01:35
02.11.2020

Tunajenga mabanda ya gharama nafuu. Piga simu 0713651858

Ep. 007. Banda Bora la kuku

347
2
0
00:08:00
07.05.2019

sifa za banda bora la kuku

Punguza Magonjwa ya Kuku kwa Kujenga Banda Bora

9321
83
5
00:00:48
17.01.2021

Changamoto kubwa kwenye Ufugaji wa kuku wa aina yeyote ile, iwe ni kuku chotara, kuku wa mayi au kuku wa nyama ujenzi wa banda ni kitu cha kuzingatia sana. Banda Bora Litahakikisha Mambo yafatayo 1. kuwapa mwanga na hewa ya kutosha, hii itasaidia mzunguko mzuri wa hewa na kuwakinga kuku wako na ugonjwa wa mafua 2. Nafasi ya kutosha, hii itawafanya kuku wapeane nafasi ya kutosha na kuwafanya wakue haraka na pia itawafanya wasidonoane. 3. Kuwatenganisha kuku na kinyesi kunasaidia kupunguza miripuko ya magonjwa. #Shorts

Назад
Что ищут прямо сейчас на
banda bora la kulelea vifaranga vya kuku g2 jankos leaked arabic dans shameem osman mojo fpga Misha shawdagor dialogue pixel 6a recenzija African zed k down malibu1 narxlari Cruise ship ЗАМУЖ ЗА БУЗОВУ ФИНАЛ ДЕШЕВАЯ ЕДА НА КАЖДЫЙ ДЕНЬ noob vs pro garrys mod noc laravel queries using query builder SAO_anime kobir laroi keyo appbar